About us

TUBONGE-TZ
UTANGULIZI.

Tubonge TZ ni blogu/tovuti ambayo inajihusisha na utoaji wa Taarifa za habari kwa jamii kwanjia ya mtando (Internet) kupitia anwani ya www.tubongetz.com . Taarifa ambazo hutolewa ni pamoja na Habari za Kitaifa, Habari za kimataifa, Biashara, Michezo na Burudani zenye maadili na zinazo gusa jamii inayo tuzunguka pasipo kupendelea upande mmoja wa chama, dini, jinsia na au rika.

Neno/Jina “TUBONGE” linamaanisha ‘TUZUNGUMZE’, Ni jina rahisi na ambalo limetokea kuwa jina pendwa ndio maana blogu hii ikaona ni vyema kuiita Tubonge TZ kwa kumaanisha “Tuzungumze Tanzania

Blogu/Tovuti hii ipo chini ya uangalizi wa watu wenye elimu ya uandishi wa habari kutoka vyuo vilivyo saliliwa vya hapa nchini Tanzania nakusababisha kuwa na habari zenye uhakika na kuaminika kwa kuhaririwa kabla ya kuwekwa kwenye tovuti ili kuifikia jamii husika.

Taarifa inayo wekwa kwenye blog/tovuti hii husambazwa kwa jamii kwakupitia mitandao ya kijamii ambayo imechukuwa nafasi kubwa sana kwa jamii ya Watanzania nakusababisha habari kusambaa kwa uraisi Zaidi hata kupita Magazeti, Redio na Runinga. Mitandao ya kijamii tunayo tumia kuweka habari zetu nipamoja na mtandao wa Facebook, Twitter na Google kupitia Google+ (Google Plus).

KANUNI NA SHERIA.

Blogu/Tovuti hii niyakijamii hivyo inaendeshwa na taratibu na kanuni ambazo hazita sababisha kumkwaza mtu kwa namna moja au nyingine isiyo ya kustahiki.

  • ·         Blogu haiweki taarifa yeyote ya uongo, uzushi au ambazo sio za uhakika ili tu kupata wasomaji wengi au kufanya ushabiki wakitu/jambo Fulani. Habari zote ambazo zitakuwa zimewekwa kwenye blogu hii zitakuwa zimefuatiliwa kwa kina na kuhakikiwa kuwa zina ukweli ndani yake ndipo zitawekwa kwaajili ya msomaji kuisoma habari hiyo.
  • ·         Blogu haitoweka taarifa ya uchochezi wa aina yeyote ile ili kusababisha kupoteza Amani kwa jamii Fulani. Habari ambazo zitasababisha uchochezi wa Siasa, Dini, Jamii, Jinsia na au Rika nakusababisha fujo blogu hii haitakuwa tayari kuiweka habari hiyo.
  • ·         Blogu hii haijuhusishi na ubaguzi wa Vyama, Dini, Jinsia, Kabila, Rika au Hali (Ulemavu wa aina yeyote ile). Hivyo taarifa inayo wekwa kwenye tovuti hii itasimamia upande wowote ule ni ilimradi kugusa jamii nakuifanya jamii nzima ifahamu ukweli wa mambo na kusaidia kusonga mbele ki fikra na uchumi.
  • ·         Masuala yote ya uzalilishaji wa Kijinsia na au Kitamaduni blogu hii haitajihusisha na kufanya hivyo bali huonya na kukemea masuala la unyanyasaji na uonevu kwa jamii nzima ili kuweka usawa na Amani kwa kila mmoja wetu anaye tuzunguka.
  • ·         Hati miliki ya kazi ya mtu, Blogu/Tovuti hii inalinda haki miliki ya kazi binafsi na au ya kundi flani. Hivyo hatujihusishi na kuweka kazi isiyo kuwa sahihi kuwekwa hadharani au kutumiwa na jamii nzima. Mfano Ku pakuwa (Download) kwazi ya msanii bila kibali chake, Kuweka nakala ya kitabu bila idhaa ya mtunzi, Kuweka habari kutoka kwenye Blogu/Tovuti nyingine bila ya kuweka hati miliki yake. Tunaheshimu kazi ya mtu au kundi ili nasisi tuheshimiwe kwenye kazi yetu.
  • ·         Lugha ya nidhamu ndio inayo tumika kwenye uandishi wa taarifa yoyote kwenye blogu hii. Lugha ikiwa ni Kiswahili na Kingereza pale inapo bidi. Matusi na au Keleli hazitawekwa kwenye blogu hii. Pia kama msomaji akiacha maoni (comment) yenye matusi kwenye moja ya habari pale tutakapo gundua mapema tutaiondoa ili kutunza ustaarabu.

DHUMUNI LA BLOGU HII.

Blogu inamadhumuni ya kusambaza taarifa muhimu kwa jamii kwa haraka na kwauwepesi ndio maana ikaamuwa kutumia njia ya mtandao ambapo jamii kubwa sasa imekuwa ikiperuzi taarifa mbali mbali kwenye mitandao kuliko kusoma kwenye Magazeti, Kusikiliza Radio na au Kutizama Runinga.
Imekuwa ni rahisi mtu kuweza kusoma habari yeyote kwenye simu yake ya kiganjani au kuperuzi habari kwenye Computer na au Tablet.

Blogu pia ina dhumuni ya kukuza na kutangaza soko la kazi za hapa nyumbani Tanzania. Ikiwa ni pamoja na kutangaza kazi za wasanii wa aina yote, kutangaza biashara ndogo ndogo na kubwa pamoja na shughuli za kijamii ikiwemo kilimo, ufugaji, uvuvi, uwashi nk.

SHUGHULI NYINGINE.
Mbali na shughuli za kuhabarisha jamii, pia tunajihusisha nakufanya maboresho ya muonekano wa blogu (Blog Design) kutokana na uhitaji wa muhusika kwa bei nafuu na kwa mfumo mzuri ambao hautasumbuwa kufunguka kwenye mtandao ulio chini (Low Network).


Pia tunafanya design ya matangazo yote ya kwenye blogu/tovuti ambayo yapo kwenye mfumo wa graphic za kisasa.

UTAWALA.

IreneLyimo (ADMIN)
Maribwa Mauli Muyenjwa (AUTHOR)
Muyenjwa Mauli Muyenjwa (AUTHOR)

MAWASILIANO.


Name

Documentary,61,Entertainment,1527,Fashion,80,Gossip,708,Health,180,Life Style,1070,Love Zone,220,Movie,117,Music,378,News,928,Photos,271,Sports,186,Top 10,25,Video,1066,
ltr
static_page
Tubonge TZ: About us
About us
Tubonge TZ
http://www.tubongetz.com/p/about-us.html
http://www.tubongetz.com/
http://www.tubongetz.com/
http://www.tubongetz.com/p/about-us.html
true
4819136446649942822
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy